Sunday, July 9, 2017

Umezaliwa kushinda sio kushindwa


Kila wakati unapotoka kwenye usingizi tambua kwamba umezaliwa kushinda na sio kushindwa, mungu wakati anakuleta dunian alikuandaa uje kushinda na kuja kuwa mtu mkubwa sana. Umeletwa ili utimize kusudi la mungu juu ya utukufu wake juu yako kwa jinsi alivyokuumba na kukupa maarifa makubwa sana ambayo kama utayatumia basi utashinda daima.
Mungu amekupa kila aina ya uwezo ndani yako unaokuwezesha wewe kushinda na kukufanya uwe mkubwa kila siku. usikubali kitu au mtu yoyote kukutoa kwenye kusudi la maisha yako ya ushindi, pambana bila kuchoka changamoto njia ni hali ya kawaida na ndizo zitakazo kufanya uwe mkubwa kama utazikabili kweli.
Usijisikie unyonge wala kujiona huna thamani pale unapopitia magumu na kudhani mungu amekuleta ili uteseke hapana, kusudi la kuja kwako hapa duniani ni kushinda na kuwa mkubwa kila siku.
Haijalishi udogo wa elimu uliyo nayo, udogo wa mtaji, au udogo wa cheo ulicho nacho. kumbuka umezaliwa kushinda sio kushindwa. ndio maana mungu anakutaarifu juu ya kupambana na shetani ambaye kama hutakuwa imara unawez ukashindwa.
You were born orignal don’t die a copy – Jumaa saidi
Tambua kwamba umezaliwa ukiwa halisi jitahidi usife ukiwa kopi. uwezo uliyoko ndani yako ni mkubwa sana hivyo pambana kila siku , wewe ni mshindi na ni mkubwa sana.
Mungu anakuona, anakujua ndani nje hawezi kukuacha uteseke bali anachotaka mungu ni wewe kupambana bila kuchoka kwa ajili ya kusherekea ushindi wako. Umezaliwa kushinda sio kushindwa.
Usijilinganishe na wengine kwa jinsi vile walivyo navyo , tambua wale unajilinganisha nao kuna wakati walikuwa kama wewe ila wao waliamua kupambana kila siku bila kuchoka na kuupata ukubwa walio nao leo.
Jitahidi kupambana leo kesho tushuudie ukubwa wako.

JE UMEFANIKIWA KUJIUNGA NDANI YA MTANDAO HUU WA MAARIFAPROFITS TANZANIA?
Ukijiunga ndani ya mtandao huu wa Maarifaprofits Tanzania. utaweza kupata vitabu vya maarifa, Biashara na kilimo bure pamoja na makala za mafundisho zitakazo kuwa zimeandaliwa kwa ajili yako.
Kama bado hujajiunga basi unaweza kujiunga hapa kwenye hii linki  JIUNGE NA MTANDAO HUU
Je unafahamu hatua 6 muhimu za mafanikio? ambazo kama ungezijua na kuzitumia ungepata mafanikio yako kwa haraka zaidi na wakati sahihi  Bonyeza maandishi haya kupata kitabu
USHAURI: umeanzisha biashara lakini hupati wateja



Karibu sana rafiki yangu:
Habari za leo mpenzi  msomaji wa makala ndani ya mtandao wako wa mpekuziforum, ni siku nyengine njema ambayo mungu ametukutanisha siku ya leo kwa ajili ya kutenda mema. Ikumbukwe mbali na kuhainga na maswala ya kidunia dhumuni kubwa ambalo mungu amelileta kwetu ni suala la mimi na wewe kufanya ibada pamoja na kuutukuza utukufu wake kupitia sisi na si vingine.
Rafiki yangu kabla ya kuendelea mbele nadhani unakumbuka kwamba nimeazimia kukwambia ukweli kwenye kila kitu ambacho unakifanya ili uweze kukihitimisha vizuri.
Mara kwa mara nimekuwa nikipokea swali kutoka kwa baadhi ya wanachama wa mtandao huu wa maarifaprofits Tanzania , ya kwamba wameanzisha biashara au wewe umeanzisha biashara lakini wateja hawaji kwako kununua hicho unachouza.
Hili ni swali ambalo huenda linawasumbua sana watu kwenye biashara zao na ndio imekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kudhani kwamba wamerogwa.
Hakuna mtu anaeweza kukuroga kwenye biashara yako ila ni wewe mwenyewe.
Rafiki yangu Falsafa ama dhana ya biashara ni pan asana na ni ngumu sana huo ndio ukweli na ndio maana kila wakati nakwambia kwamba mafanikio ni safari ndefu sana inayohitaji kujitoa zaidi.
Biashara kuifanya kwenye makaratasi ni rahisi sana lakini kuifanya kwenye vitendo ni ngumu sana,  sio kama nakutisha ama nakukatisha tama ila napenda utambue kwamba huo ndio ukweli. Sitatumia muda wangu kuanza kukukatisha tamaa ila nitatumia muda wangu kukusaidia kwenye kila hali.
Rafiki yangu kuna maswali matatu muhimu ukiweza kuyajibu kwa ufasaha utaweza kutambua ni kwanini wateja wahaji kwenye biashara yako, usikimbilie kumtafuta mchawi, mchawi wa kwanza ni wewe mwenyewe.
Kwenye mada zitakazofata nitakuelezea kwanini nazidi kukwambia kwamba wewe ndio mchawi mkuu kwenye biashara yako.
Chunguza maswali haya kwa makini:
Je hiyo biashara unayofanya au unayotaka kuifanya inahitajika kwenye hilo eneo?
Kabla ya kuanza kufanya biashara jiulize hilo swali je biashara yako inahitajika hapo ulipo, maana ukienda kuianzisha mahali ambapo haitajiki natumbua unajisumbua hakuna mteja atakaye kuja kwako.
Utakuta mtu mahali watu wanahitaji huduma ya maji yeye anakwenda kuanzisha biashara ya saloon, huko ni kufeli kuliko wazi ambapo haitaji kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kulijua hilo , kinachoitajika ni wewe kwenda sambamba na hitaji la watu husika.
Kabla kuanzisha biashara yako fanya utafiti wa vitu gani watu wanahitaji  , ukishavijua basi vifanyie kazi.
Wateja wanao uwezo wa kulipia gharama za huduma unayotaka kutoa ama unayotoa?
Swali la pili muhimu sana na hapa ndipo palipo na  mtego ambapo wengi umewashinda kuutegua, natambua lengo la kufanya biashara ni kupata faida lakini sio kigezo cha kumfanya Yule muhitaji kushindwa kulipia gharama.
Haya yote yanatokea na kwasababu ya watu kuingia kwenye biashara kwa matakwa ya watu na sio maamuzi yao, lipo wimbi huko ama huku mtaani ambalo kila siku linawasomba vijana kwa kutokuelewa dhana vizuri ya biashara.
Utakuta vijana wapo kwenye vijiwe wakiambiana uongo eti ukifanya biashara Fulani inakulipa  na ndio imekuwa sababu ya watu kufanya biashara zisizo sahihi mahali husika. Kama kweli unataka kufanya biashara zingatia maswali haya matatu.
Rafiki yangu sababu moja wapo inayowafukuza wateja kwenye biashara yako ni ukubwa wa bei kwenye bidhaa ama huduma unazotoa, weka bei ambazo watu wataweza kulipia.
Chukua mfano wa china baada ya kuona japani wanatengeneza simu nzuri na bora lakini watu wengi hawana uwezo wa kuzinunua kwa sababu ya bei yake kuwa kumbwa ndipo mchina akaja na simu zake za bei ambayo kila mtu anaweza kulipia. Na huenda hata simu unayotumia wewe ni ya kichina.
Jitahidi rafiki yangu kuweka bei ambayo mteja ataweza kulipia.
Je ina ubora kiasi cha kujitangaza yenyewe?
Ubora kwenye biashara ni kitu cha msingi  sana  na ndio huitangaza biashara yako bila ya wewe mwenyewe kujua. Mteja anapokuja kununua bidhaa kutoka kwako ikawa na ubora basi atakusaidia kuitangaza kwa wengine na itakuwa sababu ya wateja kuja kwako kununua mahitaji yao.
Katika nchi nyingi za ulaya hawatumii simu za mchina  unajua kwanini? Ni kwasababu ya ubora wake uko chini sana , hivyo rafiki yangu jitahidi kutoa huduma bora kwa wateja wako kila siku.
Nadhani mapaka hapa nitakuwa nimejibu swali hili kwa mtindo wa maswali, nakuomba usiangaike kwa waganga angaika na maswali haya na uyapatie majibu ya kina ili uweze kuendesha biashara yako vizuri.
Kama bado unahitaji ufafanuzi zaidi usijali , najua uwelewa wetu uko tofauti sana kwani hata watoto mapacha wana D.N.A tofauti, hivyo unaweza kutuma maswali au maoni kwenye email hii maarifaprofits@gmail.com  nitakujibu kwa kadri uwezo alionipa mungu.
Ofa ya kitabu cha HATUA 6 MUHIMU ZA MAFANIKIO imebaki kwa watu wachache sana hivyo kama hujapata nakala yako unaweza kukuipata sasa. Bonyeza linki hapo chini ili uweze kukipata na uweze kukisoma kwenye simu, Pc na hata Tablates.

Monday, May 8, 2017

HUTAKIWI KUKATA TAMAA PALE MAMBO YANAPOKUWA MAGUMU
Hakuna kosa ambalo, hutakiwi kufanya kama kukata tamaa pale mambo yanapokuwa hayakuendi vizuri.
Kwasababu unafanya hali kama ilikua mbaya basi iwe mbaya zaidi.

Jambo la busara ambalo unatakiwa kulifanya katika kipindi hiki ni kujipa moyo na kuendelea kutafuta njia na mbinu za kukufanya utoke hapo ulipo.
Hapa ndiyo tunakuja kuona tofauti kati ya watu ambao ni washindi na wanashindwa, waliofanikiwa na wasiyo fanikiwa.
Watu waliofanikiwa na washindi ni wale watu ambao hawakukata tamaa pale mambo yalipokuwa mabaya, pale hali inapo onyesha kupoteza matumaini lakini wao wanaendelea kupambana,
Hakuna sumu mbaya katika maisha ya mwanadamu kama kukata tamaa, kwasababu ndiyo chanzo cha kushindwa kwa Ndoto nyingi kutotimia.
Kumbuka kufanya yafuatayo pale unapokuwa unapita kwenye hali Ngumu kimaisha kwasababu hali mbaya haziepukiki ila kinacho takiwa zaidi ni kujua namna ya kukabiliana nazo.
1. Jaribu kukumbuka kipindi ambacho ulifanikisha jambo Kubwa katika maisha yako
Huu ndiyo msingi wa kujenga fikra chanya jaribu kukumbuka kipindi ambacho ulifanya vizuri na ukatengeneza mazingira ya kufanikiwa.
2. Tambua ya kuwa hakuna hali ya kudumu
Kila jambo linamsimu wake huja na kuondoka. Kwahiyo usichanganyikiwe sana pale mambo yanakuwa hayaendi sawa
4. Hesabu mambo uliyo yafanikisha mpaka sasa hivi, jiulize umeyafanikishaje na jua kwamba hili nalo unalolipitia utalitatua pia
5. Angalia zaidi namna ya kufanya hali yako ya baadae kuwa bora kuliko kuendelea kuhesabu makosa yako
Usiendelee kujilaumu kwa makosa yaliyo kwisha kufanyika. Ila focus zaidi kwenye matokeo unayo yataka kuyapata katika maisha yako.
Hakuna kitu kizuri kinacho kuja kirahisi
_Kumbuka hakuna ambae hapitii changamoto katika maisha yake, ila wengi huishia kukataa tamaa na kupoteza muelekeo, lakini watu waliofanikiwa hupambana mpaka mwisho_
Imeandikwa Daniel yonah kwa mawasiliano      +255743001529
ULEMAVU USIWE KIGEZO CHA KUTOTIMIZA NDOTO ZAKO
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ambapo naamini itakuwa yenye faida sana kwa jamii yetu.   Ikiwa leo ni tarehe 8 ya mwezi wa tano tumebakiza miezi saba ili tuhitimishe mwaka 2017 na kuingia mwaka 2018.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza wale ambao hawajakumbwa na ufyekaji wa vyeti feki.  Pole kwa wale ambao wamekumbwa na hali hii. Kikubwa nawasihi wasikate tamaa waendelee kupambana kwani kuna maisha nje ya kazi ambayo ni mazuri sana.

Usiangalie umeumia kiasi gan bali angalia ni vitu gan unataka kwenda kufanya kwa faida ya mbeleni.
Karibu kwenye makala yetu ya leo.  Siku ya leo tunakwenda kuangalia ni namna gani tunaweza kuliondoa taifa lenye tabia ya omba omba kwa kigezo cha ulemavu.

Ulemavu ni moja ya changamoto tuliyonayo kama taifa na inayotufanya kuwa omba omba zaidi kama taifa.  zipo fikra nyingi.
 Katika dunia ya leo wapo watu ambao hawana mikono wala miguu lakini wanaishi maisha yao kwa furaha ya hali ya juu na hawajutii kabisa.

mmoja kati ya wengi ni Sesser alizaliwa Thailand, familia yake ilimtenga ndani ya kipindi cha wiki moja tu tangu azaliwe na kujikuta akilelewa mikononi mwa watu baki hadi alipofikisha umri wa miaka 15 na kujiingiza katika mambo ya mitindo kupitia kuzitangaza nguo za ndani za wanawake

Wapo wengi pamoja na na NICK ambaye yeye hana miguu wala mikono lakini ni tajiri mkubwa sana.
Hivyo uleamvu ulionao usiwe kigezo cha kukatisha ndoto zako, ulemavu wako usiwe kitege uchumi kwa wengine kwa kukubali kutembezwa jua lako na mvua yako ili watu wajipatie kipato kupita wewe.
Kawaida ya kila mwanadamu kupenda kuhurumiwa na kusaidiwa , kwa sababu hiyo wamekuwa wakisubiri msaada badala ya kupiga hatua mbele.
Na hali hii ya omba omba inazidi ni kutokana naserkali kutokuweka usawa na kutowathamini watu wenye ulemavu. wapo wenye ulemavu lakini wanaujuzu wao, kikubwa hawajui ni wapi waende au nini wafanye waweze kutimiza malengo yao.