Mungu amekupa kila aina ya uwezo ndani yako unaokuwezesha wewe kushinda na kukufanya uwe mkubwa kila siku. usikubali kitu au mtu yoyote kukutoa kwenye kusudi la maisha yako ya ushindi, pambana bila kuchoka changamoto njia ni hali ya kawaida na ndizo zitakazo kufanya uwe mkubwa kama utazikabili kweli.
Usijisikie unyonge wala kujiona huna thamani pale unapopitia magumu na kudhani mungu amekuleta ili uteseke hapana, kusudi la kuja kwako hapa duniani ni kushinda na kuwa mkubwa kila siku.
Haijalishi udogo wa elimu uliyo nayo, udogo wa mtaji, au udogo wa cheo ulicho nacho. kumbuka umezaliwa kushinda sio kushindwa. ndio maana mungu anakutaarifu juu ya kupambana na shetani ambaye kama hutakuwa imara unawez ukashindwa.
You were born orignal don’t die a copy – Jumaa saidi
Tambua kwamba umezaliwa ukiwa halisi jitahidi usife ukiwa kopi. uwezo
uliyoko ndani yako ni mkubwa sana hivyo pambana kila siku , wewe ni
mshindi na ni mkubwa sana.Mungu anakuona, anakujua ndani nje hawezi kukuacha uteseke bali anachotaka mungu ni wewe kupambana bila kuchoka kwa ajili ya kusherekea ushindi wako. Umezaliwa kushinda sio kushindwa.
Usijilinganishe na wengine kwa jinsi vile walivyo navyo , tambua wale unajilinganisha nao kuna wakati walikuwa kama wewe ila wao waliamua kupambana kila siku bila kuchoka na kuupata ukubwa walio nao leo.
Jitahidi kupambana leo kesho tushuudie ukubwa wako.
JE UMEFANIKIWA KUJIUNGA NDANI YA MTANDAO HUU WA MAARIFAPROFITS TANZANIA?
Ukijiunga ndani ya mtandao huu wa Maarifaprofits Tanzania. utaweza kupata vitabu vya maarifa, Biashara na kilimo bure pamoja na makala za mafundisho zitakazo kuwa zimeandaliwa kwa ajili yako.
Kama bado hujajiunga basi unaweza kujiunga hapa kwenye hii linki JIUNGE NA MTANDAO HUU
Je unafahamu hatua 6 muhimu za mafanikio? ambazo kama ungezijua na kuzitumia ungepata mafanikio yako kwa haraka zaidi na wakati sahihi Bonyeza maandishi haya kupata kitabu
0 comments: