Karibu sana rafiki yangu:
Habari za leo mpenzi msomaji
wa makala ndani ya mtandao wako wa mpekuziforum, ni siku
nyengine njema ambayo mungu ametukutanisha siku ya leo kwa ajili ya
kutenda mema. Ikumbukwe mbali na kuhainga na maswala ya kidunia dhumuni
kubwa ambalo mungu amelileta kwetu ni suala la mimi na wewe kufanya
ibada pamoja na kuutukuza utukufu wake kupitia sisi na si vingine.
Rafiki
yangu kabla ya kuendelea mbele nadhani unakumbuka kwamba nimeazimia
kukwambia ukweli kwenye kila kitu ambacho unakifanya ili uweze
kukihitimisha vizuri.
Mara
kwa mara nimekuwa nikipokea swali kutoka kwa baadhi ya wanachama wa
mtandao huu wa maarifaprofits Tanzania , ya kwamba wameanzisha biashara
au wewe umeanzisha biashara lakini wateja hawaji kwako kununua hicho
unachouza.
Hili
ni swali ambalo huenda linawasumbua sana watu kwenye biashara zao na
ndio imekuwa sababu ya wafanyabiashara wengi kukimbilia kwa waganga wa
kienyeji kudhani kwamba wamerogwa.
Hakuna mtu anaeweza kukuroga kwenye biashara yako ila ni wewe mwenyewe.
Rafiki
yangu Falsafa ama dhana ya biashara ni pan asana na ni ngumu sana huo
ndio ukweli na ndio maana kila wakati nakwambia kwamba mafanikio ni
safari ndefu sana inayohitaji kujitoa zaidi.
Biashara kuifanya kwenye makaratasi ni rahisi sana lakini kuifanya kwenye vitendo ni ngumu sana, sio
kama nakutisha ama nakukatisha tama ila napenda utambue kwamba huo ndio
ukweli. Sitatumia muda wangu kuanza kukukatisha tamaa ila nitatumia
muda wangu kukusaidia kwenye kila hali.
Rafiki
yangu kuna maswali matatu muhimu ukiweza kuyajibu kwa ufasaha utaweza
kutambua ni kwanini wateja wahaji kwenye biashara yako, usikimbilie
kumtafuta mchawi, mchawi wa kwanza ni wewe mwenyewe.
Kwenye mada zitakazofata nitakuelezea kwanini nazidi kukwambia kwamba wewe ndio mchawi mkuu kwenye biashara yako.
Chunguza maswali haya kwa makini:
Je hiyo biashara unayofanya au unayotaka kuifanya inahitajika kwenye hilo eneo?
Kabla
ya kuanza kufanya biashara jiulize hilo swali je biashara yako
inahitajika hapo ulipo, maana ukienda kuianzisha mahali ambapo haitajiki
natumbua unajisumbua hakuna mteja atakaye kuja kwako.
Utakuta
mtu mahali watu wanahitaji huduma ya maji yeye anakwenda kuanzisha
biashara ya saloon, huko ni kufeli kuliko wazi ambapo haitaji kwenda kwa
mganga wa kienyeji ili kulijua hilo , kinachoitajika ni wewe kwenda
sambamba na hitaji la watu husika.
Kabla kuanzisha biashara yako fanya utafiti wa vitu gani watu wanahitaji , ukishavijua basi vifanyie kazi.
Wateja wanao uwezo wa kulipia gharama za huduma unayotaka kutoa ama unayotoa?
Swali la pili muhimu sana na hapa ndipo palipo na mtego
ambapo wengi umewashinda kuutegua, natambua lengo la kufanya biashara
ni kupata faida lakini sio kigezo cha kumfanya Yule muhitaji kushindwa
kulipia gharama.
Haya
yote yanatokea na kwasababu ya watu kuingia kwenye biashara kwa matakwa
ya watu na sio maamuzi yao, lipo wimbi huko ama huku mtaani ambalo kila
siku linawasomba vijana kwa kutokuelewa dhana vizuri ya biashara.
Utakuta vijana wapo kwenye vijiwe wakiambiana uongo eti ukifanya biashara Fulani inakulipa na
ndio imekuwa sababu ya watu kufanya biashara zisizo sahihi mahali
husika. Kama kweli unataka kufanya biashara zingatia maswali haya
matatu.
Rafiki
yangu sababu moja wapo inayowafukuza wateja kwenye biashara yako ni
ukubwa wa bei kwenye bidhaa ama huduma unazotoa, weka bei ambazo watu
wataweza kulipia.
Chukua
mfano wa china baada ya kuona japani wanatengeneza simu nzuri na bora
lakini watu wengi hawana uwezo wa kuzinunua kwa sababu ya bei yake kuwa
kumbwa ndipo mchina akaja na simu zake za bei ambayo kila mtu anaweza
kulipia. Na huenda hata simu unayotumia wewe ni ya kichina.
Jitahidi rafiki yangu kuweka bei ambayo mteja ataweza kulipia.
Je ina ubora kiasi cha kujitangaza yenyewe?
Ubora kwenye biashara ni kitu cha msingi sana na
ndio huitangaza biashara yako bila ya wewe mwenyewe kujua. Mteja
anapokuja kununua bidhaa kutoka kwako ikawa na ubora basi atakusaidia
kuitangaza kwa wengine na itakuwa sababu ya wateja kuja kwako kununua
mahitaji yao.
Katika nchi nyingi za ulaya hawatumii simu za mchina unajua
kwanini? Ni kwasababu ya ubora wake uko chini sana , hivyo rafiki yangu
jitahidi kutoa huduma bora kwa wateja wako kila siku.
Nadhani
mapaka hapa nitakuwa nimejibu swali hili kwa mtindo wa maswali,
nakuomba usiangaike kwa waganga angaika na maswali haya na uyapatie
majibu ya kina ili uweze kuendesha biashara yako vizuri.
Kama
bado unahitaji ufafanuzi zaidi usijali , najua uwelewa wetu uko tofauti
sana kwani hata watoto mapacha wana D.N.A tofauti, hivyo unaweza kutuma
maswali au maoni kwenye email hii maarifaprofits@gmail.com nitakujibu kwa kadri uwezo alionipa mungu.
Ofa
ya kitabu cha HATUA 6 MUHIMU ZA MAFANIKIO imebaki kwa watu wachache
sana hivyo kama hujapata nakala yako unaweza kukuipata sasa. Bonyeza
linki hapo chini ili uweze kukipata na uweze kukisoma kwenye simu, Pc na
hata Tablates.
0 comments: