Monday, May 8, 2017

ULEMAVU USIWE KIGEZO CHA KUTOTIMIZA NDOTO ZAKO

Habari za leo rafiki yangu?
Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ambapo naamini itakuwa yenye faida sana kwa jamii yetu.   Ikiwa leo ni tarehe 8 ya mwezi wa tano tumebakiza miezi saba ili tuhitimishe mwaka 2017 na kuingia mwaka 2018.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza wale ambao hawajakumbwa na ufyekaji wa vyeti feki.  Pole kwa wale ambao wamekumbwa na hali hii. Kikubwa nawasihi wasikate tamaa waendelee kupambana kwani kuna maisha nje ya kazi ambayo ni mazuri sana.

Usiangalie umeumia kiasi gan bali angalia ni vitu gan unataka kwenda kufanya kwa faida ya mbeleni.
Karibu kwenye makala yetu ya leo.  Siku ya leo tunakwenda kuangalia ni namna gani tunaweza kuliondoa taifa lenye tabia ya omba omba kwa kigezo cha ulemavu.

Ulemavu ni moja ya changamoto tuliyonayo kama taifa na inayotufanya kuwa omba omba zaidi kama taifa.  zipo fikra nyingi.
 Katika dunia ya leo wapo watu ambao hawana mikono wala miguu lakini wanaishi maisha yao kwa furaha ya hali ya juu na hawajutii kabisa.

mmoja kati ya wengi ni Sesser alizaliwa Thailand, familia yake ilimtenga ndani ya kipindi cha wiki moja tu tangu azaliwe na kujikuta akilelewa mikononi mwa watu baki hadi alipofikisha umri wa miaka 15 na kujiingiza katika mambo ya mitindo kupitia kuzitangaza nguo za ndani za wanawake

Wapo wengi pamoja na na NICK ambaye yeye hana miguu wala mikono lakini ni tajiri mkubwa sana.
Hivyo uleamvu ulionao usiwe kigezo cha kukatisha ndoto zako, ulemavu wako usiwe kitege uchumi kwa wengine kwa kukubali kutembezwa jua lako na mvua yako ili watu wajipatie kipato kupita wewe.
Kawaida ya kila mwanadamu kupenda kuhurumiwa na kusaidiwa , kwa sababu hiyo wamekuwa wakisubiri msaada badala ya kupiga hatua mbele.
Na hali hii ya omba omba inazidi ni kutokana naserkali kutokuweka usawa na kutowathamini watu wenye ulemavu. wapo wenye ulemavu lakini wanaujuzu wao, kikubwa hawajui ni wapi waende au nini wafanye waweze kutimiza malengo yao.

0 comments: